#Local News

RUTO AMPONGEZA OKOWA KWA KUCHAGULIWA TENA ICJ

Rais William Ruto amempongeza mwanasheria wa Kenya Profesa Phoebe Okowa kufuatia kuchaguliwa tena kuwa jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ, kwa muhula kamili wa miaka tisa.

Katika taarifa aliyochapisha kwenye mtandao wa X , Ruto amesema ushindi wa Okowa ni fahari kubwa kwa Kenya na utambuzi wa utaalamu wa nchi katika masuala ya sheria.

Rais amesema ushindi huo unaonyesha imani ya jumuiya ya kimataifa kwa wataalamu wa Kenya na mchango wao katika masuala ya kimataifa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *