MAHAKAMA NA POLISI WALAUMIANA KUHUSU VURUGU ZA KISIASA
Zikiwa zimesalia siku 278 kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027, mvutano umeibuka kati ya Idara ya Mahakama na Huduma ya Kitaifa ya Polisi kuhusu kuongezeka kwa magenge yanayohusishwa na vurugu za kisiasa nchini.
Jaji Mkuu Martha Koome amezitaka idara za usalama kuacha kulenga wahalifu wa ngazi za chini pekee na badala yake kuwakamata wafadhili na wafadhili wakuu wanaodaiwa kufadhili makundi hayo.
Kwa upande mwingine, maafisa wa polisi na baadhi ya viongozi wa kisiasa wameilaumu mahakama kwa kuwaachilia washukiwa kwa dhamana nafuu, wakidai hatua hiyo huruhusu wanaohusishwa na vurugu kurejea mitaani na kuendeleza uhalifu.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 









































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































