#Local News

ODM YAITA KALONZO NA MATIANG’I KUJIUNGA NAYO

Chama cha ODM kimeanzisha tena juhudi za kuvutia viongozi wa kisiasa, kikiwataka kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka na aliyekuwa Waziri Fred Matiang’i kujiunga nacho kabla ya uchaguzi wa 2027.

Katika hafla ya hivi karibuni, viongozi wa ODM wameyasuta baadhi ya makundi ya upinzani kwa kuwatenga Kalonzo na Matiang’i katika maandalizi ya uchaguzi wa urais, huku chama hicho kikisisitiza umuhimu wa ushirikiano.

Wito huo umejiri wakati ODM ikimkaribisha rasmi aliyekuwa Seneta wa West Pokot Samuel Poghisio, aliyehama chama cha KANU.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *