NYAMITA ATABIRI MPASUKO NDANI YA UPINZANI
Mbunge wa Uriri Mark Nyamita ametabiri mzozo mkubwa ndani ya upinzani, akiwashutumu baadhi ya viongozi kwa kumuunga mkono aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua licha ya kushiriki katika mchakato wa kumwondoa madarakani.
Nyamita amesema viongozi hao wanajipanga kisiasa pamoja na Gachagua baada ya hapo awali kuunga mkono kuondolewa kwake, hatua aliyosema inazua maswali kuhusu msimamo wao wa kisiasa.
Akizungumza katika mahojiano na kituo kimoja cha runinga, mbunge huyo pia alitilia shaka msimamo wa upinzani kuhusu utawala wa sheria, akitaja kinaya katika ushirikiano wa sasa kati ya Gachagua na baadhi ya washirika wake.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 













































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































