#Local News

RUTO AAHIDI MIKOPO NAFUU KWA WAZALISHAJI

Rais William Ruto ameahidi mikopo nafuu na motisha mpya kwa wazalishaji wa bidhaa nchini, katika juhudi za kuharakisha ukuaji wa viwanda na kuongeza uzalishaji wa ndani.

Akizungumza katika Mkutano wa Uzalishaji Viwandani, Ruto amesema serikali inalenga kuvutia wawekezaji, kukuza uzalishaji wa bidhaa za humu nchini na kupanua masoko ya mauzo ya nje.

Hata hivyo, sekta ya viwanda inachangia asilimia 7.1 pekee ya uchumi wa Kenya, huku serikali ikilenga kuongeza mchango huo hadi asilimia 20 ifikapo mwaka 2030.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *