#Athletics #Sports

OBIRI AJIPANGA UPYA BAADA YA KUPOTEZA TAJI LA NEW YORK MARATHON

Mwanariadha Hellen Obiri amesema atajipanga upya kwa msimu wa 2027 baada ya kushindwa kutetea taji lake la mbio za New York City Marathon Jumapili, akimaliza katika nafasi ya tatu.

Obiri, mwenye umri wa miaka 36, amekiri kuwa maandalizi yake yaliathiriwa na jeraha la kifundo cha mguu alilopata katikati ya Julai, lililomkatiza mazoezi na kumpa muda mfupi wa kujiandaa kwa mashindano hayo.

Mkenya huyo alitumia saa 2 dakika 24 na sekunde 43, sekunde moja nyuma ya Jessica McClain wa Marekani, huku Sheila Chepkirui akitwaa ushindi kwa muda wa saa 2 dakika 24 na sekunde 36.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *