#Rugby #Sports

OTUOMA AFICHUA SIRI YA USHINDI WA RISING LIONESSES

Kocha wa Rising Lionesses Knight Otuoma amesema maandalizi makini na kuwa na kikosi chenye wachezaji wengi wenye uwezo vilichangia ushindi wa kihistoria wa medali ya dhahabu katika Michezo ya Olimpiki ya Vijana ya Dakar 2026 nchini Senegal.

Kenya iliilaza Australia alama 17 kwa 12 katika fainali ya kusisimua, baada ya kusawazisha dakika za mwisho na kulazimisha mchezo kuingia muda wa ziada kabla ya kupata alama za ushindi.

Otuoma amesema mabadiliko ya kimkakati katika kikosi yalisaidia kuwapumzisha baadhi ya wachezaji kwa mechi muhimu, akisema ushindi huo unaonyesha kina cha vipaji katika raga ya Kenya na kutoa matumaini kwa mustakabali wa timu hiyo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *