OBURU OGINGA ATANGAZA KUREJEA SIASANI
Kiongozi wa ODM Oburu Oginga Odinga amesema taarifa za uongo zilizodai amefariki alipokuwa hospitalini zilimpa nguvu na azma zaidi ya kupambana na ugonjwa uliokuwa ukimsumbua
Oburu amesema anaendelea kupata nafuu na kuimarika kila siku, alipokuwa akipokea Spika wa Bunge la Taifa Moses Wetang’ula na Spika wa Seneti Amason Kingi
Oburu amesema ugonjwa wake ulipunguza shughuli zake za
kisiasa, lakini amesisitiza kuwa anatarajia kurejea katika ulingo wa siasa hivi karibuni
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 

















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































