GACHAGUA APUNGUZA WASIWASI KUHUSU MIGAWANYIKO UPINZANI
Kiongozi wa chama cha DCP Rigathi Gachagua amepuuza madai ya migawanyiko ndani ya upinzani, akisema tofauti za viongozi ni za kawaida wanapojenga muungano kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Gachagua ameelezea mvutano huo kama ushindani wa kawaida kati ya ndugu, akisisitiza kuwa viongozi hao bado wana lengo moja licha ya kutofautiana kisiasa.
Amesema upinzani hatimaye utakubaliana kuhusu mgombea mmoja wa urais atakayebeba bendera ya muungano katika uchaguzi ujao.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 

















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































