#Local News

NYORO APINGA MFUMO WA GACHAGUA

Mbunge wa Kiharu na kiongozi wa People’s Party of Kenya Ndindi Nyoro amepinga mfumo unaopendekezwa na kiongozi wa DCP Rigathi Gachagua wa kumpata mgombea mmoja wa urais kwa upinzani kuelekea uchaguzi wa 2027.

Nyoro ameonya kuwa masharti magumu na kutegemea idadi ya wafuasi pekee kunaweza kuvuruga umoja wa upinzani na kumpa Rais William Ruto nafasi rahisi ya kutafuta muhula wa pili.

Amesema uteuzi huo unapaswa kuzingatia uwezo wa mgombea kuvutia wananchi wengi, uongozi bora na kuelewa changamoto za kiuchumi zinazowakabili Wakenya, msimamo unaotofautiana na mfumo unaosukumwa na mrengo wa Gachagua.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *