#Football #Sports

LIVERPOOL YAPOTEZA REKODI YAKE ULAYA

Liverpool imepoteza rekodi yake ya kutoshindwa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuangushwa mabao 3-2 na Fenerbahce nchini Uturuki, licha ya Trey Nyoni na Alexander Isak kuifungia timu hiyo mabao.

Fenerbahce ilisawazisha mara mbili kupitia mkwaju wa Mason Greenwood uliobadilisha mwelekeo na bao la Archie Brown, kabla ya Vedat Muriqi kufunga bao la ushindi. Liverpool ilikuwa imeingia kwenye mchezo huo ikilenga kujirekebisha baada ya kupoteza dhidi ya Arsenal katika Ligi Kuu ya England.

Katika mechi nyingine, Real Madrid iliendeleza rekodi yake ya ushindi baada ya kuilaza AEK kwa mabao 3-2, huku Kylian Mbappe akisawazisha na Federico Valverde kufunga bao la ushindi dakika za nyongeza. Arsenal nayo iliifunga Slavia Prague mabao 2-1 ugenini, huku Manchester City pia ikipata ushindi ugenini wa mabao 3-2 dhidi ya RB Leipzig ya Ujerumani.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *