#Local News

RUTO AMTUHUMU GACHAGUA KWA UNYANG’ANYI

Rais William Ruto ameendeleza mashambulizi ya kisiasa dhidi ya aliyekuwa naibu wake Rigathi Gachagua, akimtaja kama kinara wa unyang’anyi wakati wa ziara yake katika kaunti za Kisii na Nyamira.

Ruto amedai kuwa Gachagua amegeuza chama chake cha DCP kuwa soko la kisiasa, ambako wanaotafuta tiketi za uchaguzi na nyadhifa mbalimbali hulazimishwa kutoa mamilioni ya pesa ili kupata upendeleo.

Ruto pia amesema kuwa alimchagua Gachagua kuwa mgombea mwenza wake kwa sababu ya kumhurumia, licha ya kile alichokitaja kuwa historia yake ya kuwanyonya wengine.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *