#Football #Sports

ALISSON ATAKA KUONGEZEWA MKATABA LIVERPOOL

Mlinda lango wa Liverpool, Alisson Becker, ameitaka klabu hiyo kumpa mkataba mpya utakaomwezesha kuendelea kuitumikia timu hiyo zaidi ya msimu huu, akisisitiza kuwa angependa kuongeza muda wake katika uwanja wa Anfield

Mchezaji huyo wa Brazil amekuwa mhimili muhimu katika mafanikio ya Liverpool tangu kujiunga nayo akitokea Roma mwaka 2018, akichangia klabu hiyo kutwaa mataji ya Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Alisson mwenye umri wa miaka 34 ameichezea Liverpool mara 347 na kushinda mataji saba makubwa, huku mkataba wake wa sasa ukitarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *